Mafunzo ya Kiswahili

Karibu kila mtu anajua msemo wa  "Hakuna matata" -
mafunzo yetu yanapeana uwezo wa kujifunza zaidi!

 

Kiswahili ni lugha ambayo imetambaa kila mahali katika Afrika Mashariki. Ikiwa ni Kenya, Tanzania, Zanzibar na nchi zingine pia - Kiswahili ni lugha ya pili inayojulikana sana katika Afrika Mashariki. Ni rahisi kujifunza, kama herufi na utamshi wake ni mwepesi sana na herufi zake ziko Kilatini. Ukifahamu gramma, hautakua na tatizo lolote kwa kuelewa.

Wanafunzi hawatojifunza lugha pekee, na pia wataweza kujua mengi kama upande wa siasa, uchumi, hadithi na utamaduni wa Afrika Mashariki.

 

Ni nani atajifunza Kiswahili?

Ukijua Kiswahili ni faida na daraja kubwa kwa yoyote anayetembelea Afrika Mashariki. Ikiwa umtaalii, mfanyabiashara, mfanyakazi wa maendeleo au mwanafunzi - maneno machache ya Kiswahili yatafungua myoyo ya watu utakao kutana nao. Utakua na urahisi sana kufahamiana na watu, kuweza kujua nchi katika ncha tofauti na utapata kujua mengi yasiosahaulika ya kipekee.

 

Mafunzo ya Kiwahili yanapatikaniwa wapi?

Kwa wanaoanza ambao wanaishi Ujerumani tunawashauri wajiunge na mafunzi ya Kiswahili katika Volkshochschule Schweinfurt (Volkshochschule = shule ya maendeleo). Mwalimu ni Hassan Abdalla kutoka kwa A.T.T. Center. Hii ni sehemu ya kujiandikisha katika wavuti wa VHS

Pia kuna uwezekano mwengine wa kuweza kujifunza Kiswahili kipekee au katika kikundi kidogo. Bei na yaliyomo katika mafunzo yetu itategemea na idadi ya wanafunzi, ni muda gani wa mafunzo, na mengineo. Tafadhali uliza kwa maelezo zaidi au tuma maombi yako kwa njia ya hewa.