A.T.T. Center imebuniwa zaidi ya miaka 20. Kwa shuguli za Ujerumani na Kenya, tunatoa huduma kwa upana na wingi, kuanzia shirika la usafiri, shirika la utafsiri, shirika la kompyuta kwa jumla, na shirika la wavuti na marketing.

 

A.T.T. Tawi la Kenya linatoa huduma zifuatazo:

 

 • Mawakala wa mashamba na nyumba:
  Ukiwa unataka kukodisha, kununua au kuuza nyumba au shamba kwa makazi au biashara, haswa nchini Kenya, sanasana katika kaunti ya Mombasa, tutafurahi kutoa huduma zetu kwa kina.

 • Eneo la biashara la A.T.T.:
  Eneo la biashara la A.T.T. linapatikana kaskazini mwa mji wa Mombasa, kando ya barabara ya zamani ya Malindi, Bamburi. Biashara zilizoko ni kama vile ya chakula, saluni za urembo, mapambo ya mwili, ushonaji nguo, huduma za fedha na kadhalika.
  Ukihitaji kukodisha mlango wa duka, tafadhali wasiliana nasi.

 • Huduma za Karani:
  Ofisi yetu itakuandikia barua zako na karatasi za kazi kwa kampuni na afisi za sheria. Utakapo hitaji, tunaweza kukutengezea vichwa vya barua zako na stakabadhi zengine zinazo hitaji kuwekewa vichwa kwa tarakilishi yetu.

 • Tafsiri:
  Huduma za tafsiri i zilizo hitimu kwa tafsiri rasmi/stakabadhi za sheria/makubaliano ya kandarasi, karatasi za maelezo, na kadhalika; kwa lugha zote.

 • Kijiji cha A.T.T.:
  Ukipendezwa kuwa na uhusiano wa karibu na wenyeji wa kijiji, tunakodisha vyumba au sehemu za kuchomea nyama [barbequeue] katika mazingara jirani ya uswahili Mombasa. Familia ya Abdallah yawakaribisha nyumbani kwao na kupanga maonyesho tofauti ya karibu kama vile, Bamburi Nature Trail, Mamba Village au kisiwa hifadhi ya bahari cha Wasini. Kwa apendaye utamaduni, kuna maonyesho tofauti ya mji wa zamani wa Mombasa na Fort Jesus au Malindi kwa magofu ya Gede, yaliyokuwa makaazi ya zamani ya waarabu katika pwani ya afrika mashariki. Safari za kutembelea mbuga nyingi za wanyama wa pori pia hupangwa.Unapotizama simba, ndovu, twiga, pundamilia, swala na wanyama mwitu wa afrika nzima kwa macho yako hukuacha na ukumbusho mzuri.

 • Kazi ya kujitolea:
  Mradi unaoendelea ni ule wakuwaekea wale wanaojitolea kufanya kazi bila malipo nchini Kenya, kama vile kwa warsha za walemavu au shule / ulezi wa mchana kwa watoto wadogo katika mitaa ya Bombolulu.

 

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na A.T.T. Center:

 

A.T.T. Center Kenya A.T.T. Center Germany
Old Malindi Rd, Bamburi-Kiembeni Apostelgasse 14
P.O.Box 88266-80100 Mombasa D-97421 Schweinfurt
Simu:  +254 (0)202310163 Simu: +49 (0)9721 185069
Mobili: +254 (0)792772795 Fax: +49 (0)9721 24763
Mobili: +254 (0)734644297 Mobili: +49 (0)171 3822911
E-mail: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. E-mail: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.