Tawi la Kenya

-Tawi la Kenya-

 

A.T.T. Tawi la Kenya linatoa huduma zifuatazo:

 

Eneo la biashara la A.T.T.:

A.T.T. Shopping CenterEneo la biashara la A.T.T. liko katika upande wa Old Malindi Road, Bamburi. Tuko na huduma tofauti za kibiashara kama maduka ya kawaida yanayotoa huduma kama: duka la vyakula, vinywagi na bidhaa za uraibu; saluni ya urembo na mapambo ya mwili; duka la madawa; duka la vifaa vya magari; baa na mgahawa; huduma za fedha (M-PESA) na kadhalika.

Ukihitaji kukodisha mlango wa duka, tafadhali wasiliana nasi.

 

Mawakala wa mashamba na nyumba:

A.T.T. Real EstateUkiwa unataka kukodisha, kununua au kuuza nyumba au shamba kwa makazi au biashara, haswa nchini Kenya, sanasana katika kaunti ya Mombasa, tutafurahi kutoa huduma zetu kwa kina.

Tafadhali wasiliana nasi kwa maelezo zaidi, au jiangalilie mwenyewe katika mtandao wetu.

 

Huduma za Karani:

Ofisi yetu itakuandikia barua zako na karatasi za kazi kwa kampuni na afisi za sheria. Utakapo hitaji, tunaweza kukutengezea vichwa vya barua zako na stakabadhi zengine zinazo hitaji kuwekewa vichwa kwa tarakilishi yetu.

 

Tafsiri:

Huduma za tafsiri i zilizo hitimu kwa tafsiri rasmi/stakabadhi za sheria/makubaliano ya kandarasi, karatasi za maelezo, na kadhalika; kwa lugha zote.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali nenda kwa Tafsiri.

 

Kijiji cha A.T.T.:

A.T.T. VillageUkipendezwa kuwa na uhusiano wa karibu na wenyeji wa kijiji, tunakodisha vyumba au sehemu za kuchomea nyama [barbequeue] katika mazingara jirani ya uswahili Mombasa.

Familia ya Abdallah yawakaribisha nyumbani kwao na kupanga maonyesho tofauti ya karibu kama vile, Bamburi Nature Trail, Mamba Village au kisiwa hifadhi ya bahari cha Wasini. Kwa apendaye utamaduni, kuna maonyesho tofauti ya mji wa zamani wa Mombasa na Fort Jesus au Malindi kwa magofu ya Gede, yaliyokuwa makaazi ya zamani ya waarabu katika pwani ya afrika mashariki. Safari za kutembelea mbuga nyingi za wanyama wa pori pia hupangwa. Unapotizama simba, ndovu, twiga, pundamilia, swala na wanyama mwitu wa afrika nzima kwa macho yako hukuacha na ukumbusho mzuri.

 

Kazi ya kujitolea:

Mradi unaoendelea ni ule wakuwaekea wale wanaojitolea kufanya kazi bila malipo nchini Kenya, kama vile kwa warsha za walemavu au shule / ulezi wa mchana kwa watoto wadogo katika mitaa ya Bombolulu. Kwa maelezo zaidi, angalia kazi ya kujitolea

 

 

Fomu wa mawasiliano

Fomu za kushusha (PDF)